Mwakikishiwadi wa Marama Central eneobunge la Butere Ondako Maina amekanusha madai kuwa ana nia ya kuhamia chama cha ANC
Kwenye mahojiano ya moja kwa moja na kituo hiki Ondako ameyataja madai hayo kama propaganda akiapa kisalia ndani ya chama cha ODM alichotumia kushinda kiti hicho
Haya yanajiri huku fununu zikizagaa kote eneo hilo kuwa yeye pamoja na vyongozi kadhaa wanapania kuhama chama cha ODM baada ya chama hicho kudaiwa kupoteza umaarufu eneo hilo siku chache tu kabla ya uchaguzi mkuu ujao
Kuhusu masomo Ondako amesema kuwa wanashirikiana na vyongozi wa utawala eneo hilo kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi aloukalia mtihani wa darasa la nane anajiunga na kidato cha kwanza
Kiongozi huyo hata hivyo ameitaka serikali kutuma pesa kwa wakati ili kuwaruhusu wanafunzi hao kuendeleza masomo yao
Ondako ameitaka serikali vilevile kuwaruhusu watoto wao kujiunga na vyuo vya masomo ya anuwayi
By James Nadwa