Wito umetolewa kwa vijana kutoka eneobunge la Mlima Elgon na kaunti ya Bungoma kwa jumla kujiunga kwenye vyuo vya kiufundi ili kupata ujuzi utakaowawezesha kujikimu siku za usoni badala ya kutegemea kazi za ajira.

Katibu mkuu wa chama cha Ford Kenya eneobunge la Mlima Elgon Chrisandos Makokha anahoji kuwa ipo haja kwa vijana kujiunga kwenye vyuo vya kiufundi ili kupata ujuzi wa kujiajiri hasa baada ya serikali kuwekeza pakubwa kwenye vyuo hivyo.

Wakati uo huo Makokha amewataka vijana kujitenga na wanasiasa ambao nia yao ni kuwatumia ili kujifaidi huku akionekana kukashifu vurugu za mirengo ya siasa ambayo inaendelea kushuhudiwa kwenye kaunti hii.

Makokha ambaye ameonyesha nia ya kuwania kiti cha uwakilishi wadi ya Chesikaki kwa mara ya pilikwenye uchaguzi mkuu ujao amewataka wananchi kuwachagua wanasiasa kwa misingi ya ajenda ya maendeleo.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE