Viongozi wa vijana katika chama cha ODM wamejitokeza na kupinga uvumi unaoenezwa kuwa huenda naibu mwenyekiti wa chama hicho Wycliffe Oparanya akakikura chama hicho na kujiunga na mrengo wa Tangatanga.
Wakiongozwa na kiongozi wa vijana katika chama hicho kaunti ya Kakamega Moffart Mandela na Amos Liyai, wametetea Oparanya ambaye pia ni gavana wa Kakamega wakisema kile wanafahamu kila kiongozi ana haki ya kukutana na kuabadilishana mawazo kisiasa kinyume na inavyodaiwa.
Hii inajiri siku moja baada ya gavana Oparanya kuonekana kwenye mitandao akiwa ameandamana na kundi la Tangatanga maeneo ya masai mara.
By Sajida Javan