Serikali ya kaunti imeombwa kusaidia chama cha Matioli Welfare Group katika kujiendeleza na kufanikisha miradi yao.
Akizungumza katika mkutano uliowajumulisha wanachama wote wa Matioli Welfare Group katika wadi ya Chegulo kata ya Matioli kaunti ndogo ya Malava kaunti ya Kakamega,mwenye kiti wa chama hiki Daniel Mulambula ameelezea baadhi ya miradi ambayo wameanzisha naimekuwa ya kufana sana kwa wanachama wake
Mwenyekiti huyo vilevile amesema minghairi yakuanzisha miradi hiyo,kuna changamoto kadha wa kadha ambazo wanakumbana nazo na hivyo kuwataka viongozi wa eneo hilo kuingililia kati ili kufanikisha miradi yao bila ya tashwishwi yoyote
Naye Emily Nanzala ambaye ni mweka hazina katika chama hiki ametoa ushauri kwa akina mama kujiunga na vyama ili wakaweze kuinua uchumi wan chi ya kenya
Aidha, Isaac Mukanzi ambaye ni katibu wa chama amewarai vijana kutumia mda wao ipasavyo na kuwaonya dhidi ya kujihusisha na vileo na hivyo kujihusisha na mambo ya maana
By Mary Mwano