Chama cha kutetea masilahi ya walimu nchini KNUT kaunti ya Kakamega chafanya uchanguzi huku aliyekuwa mwenyekiti na katibu mkuu Patrick Chungani na Argadious Liyayi kwa mtawalia wakichaguliwa tena 

Wakizungumza baada ya kuchaguliwa afisi hiyo ya kaunti ikiongozwa na mwenyekiti wake Patrick Chungani imeahidi kuendelea kutetea masilahi ya walimu bila kuogopa vitisho kutoka kwa serikali na tume ya kuajiri walimu TSC 

Ni usemi ulioungwa mkono na katibu mkuu Argadious Liyayi na mwakilishi wa chama hicho katika kanda ya magharibi Emily Neuto waliokariri kuwa ni umoja wao tu utawezesha walimu kupata haki yao na kufanya kazi kwa mazingira bora 

 Mwakilishi wa wamama aliyechaguliwa ni Janet Wasike , Tungani Ashikhule  akiridhika na wadhifa wa naibu mwenyekiti miongoni mwa nyidhifa zingine 

BY Boaz Shitemi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE