Mbunge wa Lurambi askofu Titus Khamala amepuuzilia mbali madai ya baadhi ya viongozi eneo la Magharibi kumdhalilisha kinara wa ANC Musalia Mudavadi akisema kama jamii  wamefanya uamuzi wa kutafuta uongozi wa taifa hili

Akiongea eneo la Shitungu kwenye hafla ya kuchangisha pesa za ujenzi wa makao ya watoto yatima chini ya kanisa la Christian Apostolic Ministry eneoa Shitungu Butsotso Mashariki askofu Khamala amesema kama jamii wamepoteza mengi kwa kuwa nje ya serikali

Askofu Khamala amesema wale wanaomdunisha Mudavadi na chama cha ANC hawatafaulu katika njama yao

Askofu Khamala ameyasema haya kwenye mchango wa kusaidia ujenzi wa makao ya watoto katika eneo la Shitungu Butsotso Mashariki ambako askofu wa kanisa hilo Francis Otsialo amesema wanalenga kuwafikia watoto wenye changamoto za maisha kupitia kwa ujenzi wa makao hayo juhudi ambazo khamala ameahidi kushirikiana na mashirika ya kijamii kuinua maisha

By Lindah Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE