Viongozi wa makanisa mjini Kakamega wanamtaka rais Uhuru Kenyatta kuachia mahakama Uhuru wa kutekeleza kazi yake bila kushurutishwa
Wakiongozwa na Apostle Charles Omuroka wa Logos Celebration International Ministries Amalemba wanamtaka rais kuzingatia ushauri wa kidini kuongoza taifa
Amesema usemi wa rais wakati wa sherehe za Madaraka mjini Kisumu uliashiria vitisho kwa mahakama
Wakati uo huo Omuroka amemtaka jaji mkuu Martha Koome kusimama kidete na kuwatetea wakenya kwa mujibu wa katiba
By Linda Adhiambo