Idadi ya virusi vya korona inaendelea kuongezeka sawia na wale wanaoendelea kupona. Hii leo Visa vya walio ambukizwa virusi vya corona vimekuwa 183 na kufikisha jumla ya watu walio ambukizwa 8,250 chini ya saa ishirini na nne ambapo sampli 2,061zilifanyiwa vipimo
Waziri wa afya Dkt. Mutahi Kagwe hii leo alieleza kuwa kutoka kwa visa hivyo 183 ni kuwa 177 ni wa kenya na 6 wakiwa raia wa kigeni. Wanaume walio ambukizwa ni 119 na wanawake wakiwa 64 na huku walioambukizwa wakiwa kati ya miaka 4 na miaka 75.
Nairobi inaongoza kwa visa 100 ,machakos ikiwa na visa 37 ,kiambu visa 14 ,Mombasa visa 13 ,Kajiado visa 11 ,Nakuru visa 5 na Busia ina visa 3.
Wagonjwa 90 wameruhusiwa kwenda nyumbani na kufikisha idadi ya walio pona 2504 huku watu watatu wakiaga dunia na kufikisha idadi ya 167 waliofariki kutokana na ugonjwa huo . Waziri Kagwe amewaonya wakenya dhidi ya kuwa watepetevu hasa baada ya rais Uhuru Kenyatta kufungua usafiri kutoka kaunti moja hadi nyingine