Kufwatia ongezeko la visa vya dhulma dhidi ya watoto katika jamii haswa siku za hivi punde mshirikishi wa usalama Kanda ya magharibi Esther Maina amewaonya wazazi watakaopatikana wakihusika kwenye visa hivyo kuwa watakabiliwa kisheria
Kwenye kikao na wanahabari afisini mwake Maina amesema kuwa kama vitengo vya usalama wanafanya wawezalo kukomesha visa hivyo
Hata hivyo amewataka waathiriwa kuripoti pindi wanapotendewa unyama huo ili hatua za dharura zichukuliwe
machifu dhidi ya kusuluhisha kesi za ubakaji nje ya mahakama akisema kuwa hii inazuiya waathiriwa kupata haki
Amewataka wazazi kumakinika na usalama wa watoto wao haswa wakati huu ambapo wako nyumbani kwa likizo fupi
Haya yanajiri huku shirika lisilo la kiserikali linaloangazia dhulma dhidi ya watoto la Survivors of Child Sexual Abuse likionyesha kuwa watoto 2 kati ya 4 hunajisiwa kila siku haswa kaunti ya Kakamega huku visa zaidi ya 200 vikiripotiwa kwa muda wa miezi 3 iliyopita
Shirika Hilo aidha limedokeza kuwa wingi wa visa hukosa kuripotiwa kwani hushugulikiwa katika kiwango cha kijamii
By James Nadwa