Paris St-Germain itafikiria kumuuza mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, wa miaka 22, mwisho wa msimu huu iwapo mshindi huyo wa kombe la dunia atakataa kuandikisha kandarasi mpya na klabu hiyo. Klabu ya Liverpool na ile ya Real Madrid zina hamu ya kumsaini mshambuliaji huyo hatari.

Huku ligi Uingereza klabu ya Chelsea ina hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Borrusia Dortmund mwenye umri wa miaka 20 Erling Haaland Kutoka klabu ya Borussia Dortmund pamoja na beki wa Bayern Munich raia wa Austria David Alaba, 28, mwisho wa msimu huu .

Mchezaji huyo ambaye ni mzaliwa wa eneo la Leeds lakini mwenye uraia wa Norway, Haaland ambaye anaweza kuondoka katika klabu hiyo iwapo dau la £66m litalipwa , ananyatiwa na Real Madrid ambayo pia ni klabu ambayo inamsaka Alaba.

Ugani Emirates Beki wa Arsenal na England Ainsley Maitland-Niles Mwenye umri wa miaka 23, yuko tayari kuondoka katika klabu hiyo kwa mkopo ili kupiga jeki nafasi yake ya kushirikishwa katika kikosi cha England cha mashindano ya Ulaya yatakayofanyika majira ya joto.

Huku Mkufunzi mpya wa Chelsea Thomas Tuchel akisema kuwa  hana mipango  ya kuwasajili wachezaji wapya katika kipindi kilichosalia cha dirisha la uhamisho.

Hayo yakijiri Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta amesema kwamba atafikiria uwezekano wa kuongeza muda wa kandarasi ya mkopo ya Martin Odegaard ili kusalia katika klabu hiyo zaidi ya msimu huu baada ya kujiunga na klabu hiyo kutoka Real Madrid.

Na Liverpool inatarajiwa kumsaini mchezaji mwenye umri wa miaka 16 kiungow a Derby Kaide Gordon, ambaye ameiwakilisha England katika kiwango ha wachezaji wasiozidi umri wa miaka .

Story by Samson Nyongesa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE