Kulizuka kizaazaa kwenye mazishi ya mzee David Kweyu mango kijiji cha Makunga eneo bunge la Mumias Mashariki baada ya wafuasi wa seneta wa Kakamega Cleophas Malala kumvamia mwaniaji wa kiti cha eneo bunge la Mumias Mashariki Peter Salasia.

Hii ni baada ya Salasia kumtaka kinara wa NAC Musalia Mudavadi, Moses Wetangula na Cleophas Malala kujiondoa katika swala la kufufuliwa kwa kiwanda cha Sukari cha Mumias.

Aidha Malala alijitetea na kusema aliwasilisha mswada huo katika bunge la seneti kwa kile alichodai kuwa swala la kukabidhi kiwanda hicho kwa mfanyibishara DEVKI haukuhusisha wadau na wakazi wa eneo zima la Mumias kwa uwazi.

Huku Khalwale na Washiali wakinyoshea lawama Malala kwa kuwa mstari wa mbele, kuzuia kufufuliwa kwa kiwanda hicho ambacho kilifeli miaka kumi zilizopita.

Khalwale alitumia fursa hiyo kumtaka rais Uhuru Kenyatta kuwahapisha majaji sita waliotemwa.

By Javan Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE