Familia ambazo makaazi yao yaliteketezwa kwenye mashambuluzi ya majambazi yanayoendelea katika kaunti ya Laikipia, zinajengewa nyumba na serikali

Waziri wa usalama Fread Matiang’I alishuhudia ugawaji wa vifaa vya ujenzi na chakula kwa familia zilizo adhirika. Vilevile aliweza kuzindua divisheni ya polisi ya Ol Moran ambayo itakua na maafisa 100 wa polisi ili kupiga doria katika eneo la Laikipia Magharibi

Wakaazi wanahimizwa kurejea katika makaazi yao na kuendelea na maisha yao ya kawaida. Nyumba 29 zilipokea vifaa vya ujenzi na chakula na familia 200 ambazo ziliachwa bila makaazi.

Aidha, waziri Matiangi aliagiza shule za eneo hilo, zikiwemo zile ambazo hazijafunguliwa kwa muhula wa kwanza kurejelea masomo  huku akiwahakikishia wakaazi kuhusu usalama wa watoto wao na pia waalimu.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE