Wafanyibiashara katika soko la Ingolomosio eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega wamelalamikia ukosefu wa vyoo na maji kwenye soko hilo na kuitaka serikali ya kaunti ya Kakamega kuwajengea vyoo na maji kuzuia mkurupuko wa magonjwa yanayotokana na uchafu.
Wakiongozwa na Dinah Chenyeka wafanyibiashara hao wanasema kuwa wanapitia changamoto nyingi wanapotaka kwenda haja kwani inawabidi kwenda vichakani kujisaidia
Wakati huo uo wanasema kuwa soko hilo halina Maji ya kutumia hasa wakati huu wa corona huku wakihofia kupatwa na ugonjwa unaotokana na uchafu huku wakiitaka serikali ya kaunti ya Kakamega kuingilia kati kwani wanalipa ushuru kama wakenya wengine.
By Imelda Lihavi