Wafanyibiashara katika soko la Ebutobe eneo bunge la Mumias Magharibi kaunti ya Kakamega wamelalamikia kufanyia biashara yao kwenda giza na kufwata viongozi waliochaguliwa eneo hilo kuwawekea taa za mwangaza kwenye soko hilo.
Wakiongozwa na Boaz Mwanza na Ibrahim Ouma wanasema kuwa wanafanyia biashara zao kwenye giza na kuwataka viongozi waliochaguliwa kuingilia kati kuwaekea taa aina ya mulika mwizi.
Tunafanyia biashara kwa giza na hio ni hatari sana. Tunaona soko zingine katika hii kaunti yetu ya Kakamega ziko na taa. tunawaomba viongozi wetu hasa MCA wetu waingilie kati na wahakikishe kwamba tuko na taa katika soko hili ili tuweze kupunguza visa vya wizi katika soko hili. walisema
Wakati huo uo wafanyibiashara hao ambao ni wenyeji wa kijiji cha Elwasuna wamelalama kutelekezwa na mbunge wa eneo hilo kwa upande wa nguvu za umeme wakidai kuwa ameegemea upande mmoja.
Mbunge wetu ameegemea upande mmoja tu sisi hapa kwa kijiji cha Elwasuna hatuna hata stima tuko kwa giza hakuna maendeleo katika kijiji tunaomba mbunge wetu aweze kuangazia hiki kijiji
Juhudi za kumpapata mbunge wa eneo hilo Johnstone Naicca kutoa usemi wake ziliambulia patupu kwani hakupatikana kwenye simu.
By Richard Milimu