Walokuwa walinzi pamoja na vibarwa sokoni Harambe eneobunge la Matungu wanalilia haki kutokana na kile walichokitaja kama kulagaiwa na mwaajiri wao
Wakiongozwa Joseph Baraza vibarwa hao waamemlaumu mwanasiasa fulani kutoka Kaunti jirani kuwafanyisha kazi pasi na malipo
Licha ya kufika kwenye afisi za Leba kaunti ya KAKAMEGA na hata kutembelea MASHIRIKA mbalimbali ya kiserikali kutafuta haki wanadai kuwa juhudi zao bado hazijazaa matunda
Wafanyikazi hao wanalalamikia ugumu WA maisha ikiwemo kushindwa kuwalipia karo WATOTO wao na kusambaratika kwa ndoa zao
Juhudi zetu za kumfikia mwanasiasa HUYO zikigonga mwamba BAADA ya kukosa kushika simu zetu
By James Nadwa