kiwanda cha kusaga sukari cha Busia kilichoko wadi ya Busibwabo eneo bunge la Matayos kaunti ya Busia kutangaza kuwa huenda kikawasimamisha kazi zaidi ya wafanyakazi wake 500 kutokana na kiwanda hicho kukosa malighafi au miwa ya kutosha ya kusaga sukari, imekemewa vikali na baadhi ya wakulima wa miwa katika kaunti ya Busia.

Wakulima hao wakiongozwa na Lambat Ogochi wanasema kaunti ya Busia ina miwa ya kutosha hivyo basi wafanyikazi katika kiwanda cha Busibwabo hawapaswi kufurushwa.

Matamshi ya wakulima hawa yanajiri siku chache tu baada ya msemaji wa kiwanda cha Busia Sugar Stephen Mulla na afisa anayesimamia wafanyakazi Caleb Anyula kusema kuwa kiwanda hicho kimekosa Miwa ya kutosha baada ya Serikali kutangaza marufuku ya uagizaji Miwa kutoka nchini Uganda, hivyo basi hatua ya kuwasimamisha kazi baadhi ya wafanyakazi wake.

Ripoti ya Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE