Kulingana na wizara ya afya humu nchini visa vya corona vinaendelea kuongezeka. Hii leo visa vipya vya maambukizi ya korona ni 123 na kufikisha idadi ya walio ambukizwa ugojwa huo kuwa 98,555.

Visa hivyo vipya vimetokana na sampuli 4,948 zilizopimwa katika muda wa masaa 24 yaliyopita. Hii imefikisha jumla ya sampuli zilizopimwa humu nchini hadi 1,102,595. Visa hivyo vipya vinajumuisha Wakenya 111 na raia 12 wa kigeni, wanaume 74 na wanawake 49, wote kati ya  umri wa mwaka mmoja hadi miaka 85.

kulingana na Waziri Wa Afya Mutahi Kagwe wagojwa 412 wamepona kati yayo 378 wakiwa kwenye mpango wa kutibiwa nyumbani na 34 kutibiwa hospitalini. Jumla ya waliopona kutokana na COVID-19 kufikia sasa ni 81,667.

Wagojwa wanne wamefariki kutokana na ugonjwa wa covid 19 na kufikisha jumla ya walio fariki 1,720

Story by Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE