Wahudumu wa bodaboda kutoka eneo la Cheptais eneobunge la Mlima Elgon wameshiriki maandamano ya amani kulalamikia kile wanachodai kuhangaishwa na maafisa wa polisi wa Sirisia ambao wameweka kizuizi kwenye makutano ya barabara ya kutoka Namutokholo kuelekea Kimabole.

Wahudumu hao wa bodaboda wanahoji kuwa lengo la maafisa wa polisi kutoka Sirisia  kuweka kizuizi kwenye barabara ya Namutokholo kuelekea Kimabole  lilikuwa ni kuwawezesha maafisa wa idara ya afya kupima viwango vya joto vinavyotokana na virusi vya corona ila kwa sasa wanadaiwa kujihusisha na visa vya rushwa.

Kwa sasa wanapendekeza maafisa hao wa polisi kuondolewa eneo hilo na kuwaruhusu wahudumu wa afya kuendesha kazi yao kitaaluma.

Hata hivyo kamanda wa polisi eneo la Sirisia David Kandie ameahidi kufanya uchunguzi wa kina kufwatia lalama hizo na kuwataka viongozi wa bodaboda kuwasilisha lalama zao afisini mwake ili hatua madhubuti  zichukuliwe.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE