Wahudumu wa bodaboda kutoka wadi ya Kabuchai-Chwele eneobunge la Kabuchai kwa kauli moja wamesema watashirikiana na vyombo vya usalama kwa kudumisha amani huku wakiahidi kutokubali kutotumiwa na wanasiasa kuzua rabsha.
Wakizungumza baada ya kukutana na mwakilishi wadi ya Kabuchai-Chwele kujadili namna ya kusuluhisha tofauti zao wahudumu hao wakiongozwa na mwenyekiti wao Joel Wekesa wamesema watashirikiana na vyombo vya usalama huku wakiwataka wenzao kuwapa heshima ya kutosha viongozi wa siasa waliochaguliwa.
Aidha wamedokeza kuwa kamwe hawatokubali kutumiwa na wanasiasa kujinufaisha wakiahidi kuendeleza injili ya amani eneobunge la kabuchai.
Mwakilishi wadi ya Kabuchai-Chwele, Barasa Mukhongo akiwataka wanasiasa ambao wameonyesha nia ya kuwania viti mbalimbali eneo hilo kudumisha amani, na kumsihi mbunge wa eneo hilo majimbo kalasinga kusaidia kutatua baadhi ya changamoto wanazopitia wahudumu hao.
By Imelda Lihavi