Wakaazi eneobunge la Mumias Mashariki wametakiwa kujitokeza na kupata chanjo dhidi ya virusi vya Corona ili kujikinga kutokana na ugonjwa huo
Afisa mkuu wa afya eneo hilo la Mumias Mashariki William Malakwen amekanusha uvumi kuwa huwenda chanjo hiyo ina madhara akiitaja kuwa salama
Afisa huyo wa afya amesema kuwa wanaolengwa ni watu wazima pekee akionyesha kuridhika na namna zoezi hilo linavyoendelea eneo hilo
Kuhusu chanjo dhidi ya ugonjwa wa ukambi iliyokamilika siku chache zilizopita Malakwen amehoji kuwa zaidi ya asilimia 90 ya watoto kutoka kaunti hiyo ndogo wamepata chanjo hiyo
By James Nadwa