KWakazi wa mtaa wa Shikhambi viungani mwa mji wa Kakamega kwa mara nyingine wanaitaka idara ya usalama mjini Kakamega kuingilia kati na kukabili visa vya wizi na uhalifu kwa jumla vinavyoendelea kuwakumba.

Wakazi wamelalamikia mbinu mpya inayotumiwa na wezi ambao kwa njia moja au nyingine huweza kuingia katika nyumba za wakazi na kuwaibia mali ya maelfu ya pesa wakati wakilala bila ya wao kusikia lolote.

James Mushasha aliyeathirika na visa hivi jana usiku, anadai kuwa licha ya yeye kuufunga mlango wake kabla ya kulala aliupata mlango ukiwa wazi nyakati za alfajiri mali yake ikiwa imebebwa.

Ni visa ambavyo vimewaathiri hata maafisa wa usalama wanao ishi eneo hilo, maafisa wa nyumba kumi pia wakivamiwa na hata kuumizwa katika juhudi zao za kukabiliana navyo.


 Mwenyekiti wa nyumba kumi Reuben Otiende na naibu wake  Zablon Were wameitaka idara  ya usalama kushirikiana nao pamoja na wakazi wa mtaa huo kukabiliana na visa hivyo vya utovu wa usalama.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE