Wakaazi wa eneobunge la Sirisia wamehimizwa kuishi kwa amani na kuweka kando swala la ukabila kama njia pekee itakayosaidia kufanikisha ajenda ya maendeleo eneo hilo.

Akihutubu kwenye hafla ya mazishi eneo la Lwandanyi eneobunge la Sirisia mbunge wa eneo hilo John Koyi Waluke amehidi kuunganisha jamii zote zinazoishi eneo  hilo huku akiwataka wananchi kufanya kazi kwa karibu na serikali.

Wakati uo huo waluke ameahidi kuzidi kuboresha miundi msingi ikiwemo ukarabati wa taasisi za elimu kando na ujenzi wa barabara za eneo hilo.

Amemkashifu vikali mwakilishi wadi ya Lwandanyi Tony Barasa kwa kudaiwa kueneza uvumi kuhusu ununuzi wa basi la shule ya upili ya Machakha akimshauri kuwahudumia wakaazi wa wadi yake ipasavyo.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE