Wakaazi wa kaunti ya Bungoma wamehimizwa kuhifadhi misitu kama njia mojawepo itakayosaidia kuboresha mazingira na kuafiki asilimia kumi hitajika  kumi ya msitu humu nchini.

Ni kauli ya katibu mwandamizi katika wizara ya fedha na mipangilio Amos Wafukho akizungumza baada ya kuongozahafla ya upanzi wa miti katika msitu wa Cheptais eneobunge la Mlima Elgon ambaye amehoji kuwa hatua hiyo itasaidia kuboresha mazingira kando na kutoa suluhu dhidi ya mafuriko ambayo yamekuwa yakishuhudiwa mara kwa mara.

Kamishna wa kaunti ya Bungoma Samwel Kimiti akiwahimiza wakaazi wa eneobunge la Mlima Elgon kuzidi kudumisha amani na kuishi kwa upendo.

Naye naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Cheptais Samwel Towet akiwapongeza wanafunzi na wakaazi wa eneo hilo kwa kuitikia wito wa kupanda miti msimu huu.

Afisa wa mazingira kaunti ya Bungoma Vitalis Osodo  akidokeza kuwa tayari ekari elfu nne za msitu huo zimetwaliwa kutoka mikono ya wananchi ambao wamekuwa wakijihusisha na kulimo.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE