Wakazi wa wadi ya Marama Magharibi eneo bunge la Butere kaunti ya Kakamega wameitaka serikali ya kaunti kukamilisha miradi iliyoahidiwa na gavana Wycliffe Oparanya kabla ya kipindi chake cha kuhudumu kukamilika
Wakiongea kijiji cha Lwaminyi wakati wa kutoa maoni kuhusu maendeleo ya kaunti, wakazi hao wanasema maswala ya barabara na maji hayajashughulikiwa ipasavyo
Hata hivyo mwakilishi wa wadi hiyo Boaz Omukunde Saitama ambaye alihudhuria kikao hicho amewataka wakazi kuwa na subira akisuta uchelewashaji wa fedha za serikali
Saitama amewataka wakazi kuona kwamba wanaunga mkono BBI akisema ndio suluhu kwa changamoto za miradi mashinani