Huku bunge la kitaifa na lile la seneti likitarajiwa kujadili mswada wa marekebisho ya katiba kupitia kwa ripoti ya BBI, sasa mwakilishi wa akina mama kaunti ya Kakamega Elsie Muhanda ameisuta kamati ambayo ilitwikwa jukumu la kukusanya maoni kwa kukosa kujumuisha mgao wa fedha wa akina almarufu kama Ngaaf kwa ripoti hiyo

 Akizungumza mjini Kakamega baada ya mkutano wa mwaka na shirika moja la uwekezaji, Bi. Muhanda amesema kuwa licha wao kama akina mama wa mabunge hayo kuzuru kila kaunti kushabikia ripoti hiyo wanasikitika kuona kwamba matakwa yao ya kujumuisha hazina hiyo ya Ngaaf kwa ripoti ya BBI haikuzingatiwa jinsi walivyo pendekeza

Sasa mwakilishi wa akina mama huyo anasema iwapo ripoti ya BBI itaidhinishwa kupitia kwa kura ya maoni kwa kuondoa kiti cha akina mama wa kaunti itakuwa bora mgao huo uendelea kuwepo hata watakapokuwa kwa bunge la seneti

 Aidha mama kaunti huyo amewarai wakaazi wa kaunti hiyo kuwa wepesi kwa kujiunga kwa mashirika ili wapate kunufaika nayo

By Boaz Shitemi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE