Mshauri wa gavana wa Kakamega kuhusu maswala ya uongozi Musa Chibole amekanusha madai ya kuwepo kwa mapendeleo katika utoaji wa tenda kwenye kaunti hiyo
Kwenye mahojiano ya kipekee na idhaa hii Chibole amesema kuwa shuguli hiyo hufanywa kwa uwazi akiwataka walio na malalamishi kuwasilisha kwenye kamati simamizi
Amesema kuwa hatua zote hufwatwa kikamilifu
Amewataka wakaazi kushiriki kwenye vikao vya kutoa maoni kuhusu namana wangetaka kuhudumiwa na uongozi wa kaunti hiyo
Vilevile ametoa changamoto kwa wakaazi kuwapiga msasa vyongozi kabla ya kuwachagua
By James Nadwa