Kufwatia mvua inayozidi kunyesha sehemu tofauti nchini wakaazi wanaoishi karibu na mito na maeneo ya chemichemi za maji wilayani Khwisero wametakiwa kuhamia kwenye sehemu za miinuko ili kuepuka maafa ambayo huwenda yakaletwa na mvua hiyo
Kamishna wa kaunti ndongo ya Khwisero John Nyakwara amesema kuwa baadhi ya mito eneo hilo ukiwemo mto Yala unazidi kujaa maji na hivyo wakaazi wanafaa kuchukua tahadhari ya mapema
Kiongozi huyo amewataka wazazi kuwa makini na watoto wao haswa msimu huu wa likizo
Wazazi sasa shule zimefungwa, tieni bidii kwa kuwakuza watoto wenu kwa sababu bado wanakua na maisha yao yataharibika. kaeni na watoto nyumbani na muwafunze kazi za ziada kama kupanda mahindi, kuuza mboga sokoni na kazi zingine mingi ili wasijiuzishe na tabia mbaya na tuweze kuangamiza mimba za mapema
Kamishna huyo vilevile amewatahadharisha wazazi dhidi ya matumizi mabaya ya pesa zao kwenye likizo hii ikitiliwa mkazo kuwa wanafunzi wanafaa kurejea shuleni mwezi ujao
By James Nadwa