Huku kampeni za uchaguzi mkuu ujao zikizidi kushika kasi, shirika moja lisilokuwa la kiserikali la Western Kenya Peace Innitiative  limeanza misururu ya kuwahamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kudumisha amani ili kuzuia uwezekano wa ghasia wakati wa kampeni hizo na hata baada ya uchaguzi.

Akihutubu baada ya kutoa mafunzo kuhusu amani kwa viongozi wa wahudumu wa bodaboda kutoka kaunti ndogo ya Cheptais eneobunge la Mlima Elgon na idara ya usalama, mshirikishi wa shirika hilo mchungaji Johnstone Nyongesa amesema shirika hilo litahusisha idara mbalimbali ili kueneza ujumbe wa amani taifa linapojiandaa kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Kamishna wa kaunti ndogo ya Cheptais Samwel Towett ametaja sekta ya bodaboda kuwa nguzo muhimu ya kueneza ujumbe wa amani huku Washingtone Okubasu, aliyemwakilisha kamanda wa polisi eneo hilo akitaka kuwepo ushirikiano dhabiti ili kudumisha amani.

Nao wahudumu wa bodaboda kutoka kaunti ndogo ya Cheptais wakiongozwa na Fred Muge na Mark Matanda wakiahidi kuhubiri injili ya amani hasa baada ya kupokea mafunzo hayo.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE