Kampeni dhidi ya virusi vya korona inazidi kupamba moto huku mwananchi akishauriwa kuendelea kuzingatia masharti ya kujilinda na janga hilo bila kupuuza.

Akiwahutubia waombolezaji katika ibaada ya mazishi ya mwenda zake Shem Lutomia Sakwa katika kijiji cha Samitsi, wadi ya Shirugu-Mugai  eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega, chifu wa lokesheni ya Shirugu Simon Swani anawaomba wakaaji kutilia maanani masharti hayo.

Anawaonya wanaokiuka sheria hizo kwamba watatiwa mbaroni wakipatikana.

Vilevile anawauliza viongozi wa makanisa maeneo hayo kuendesha ibaada za ndani ya kanisa kwa kuzingatia saa zinazohitajika kufikia saa sita za mchana la sivyo atakayetiwa mbaroni ni mchungaji wa kanisa.

Ni ibaada iliyoendeshwa chini ya masharti ya covid-19 ambayo ilihudhuriwa pia na wawakilishi wa viongozi wa kisiasa.

By Wycliffe Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE