Wakaazi wa kijiji cha imakuchi katika lokesheni ndogo ya Ivakale
Lokesheni ya kambiri eneo bunge la Shinyalu, wanaombwa
Kutochukulia mzaha agizo la kufika kwenye baraza.
Akiongea na kituo hiki baada ya wakaazi hao kutofika katika baraza
Lililoitishwa hii leo ijuma katika kanisa la marafiki la Mungakha, mzee
Wa mtaa wa Imakuchi Evans Lisanza Mmayi anasema kwamba baraza
Hilo limeitishwa kufwatia pendekezo lake mjumbe wa Shinyalu Kizito
Mugali la kujenga shule mpya maeneo hayo.
Hata hivyo amewarai kufika kwenye baraza juma lijalo siku ya
Jumanne tarehe 16 asubuhi saa tatu ili kujadili swala hilo.
Story by Sajida Wycliffe