Siku moja baada ya tume ya IEBC kuidhinisha sahihi kupisha mchakato wa BBI ,katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin sifuna amesema Kwa sasa kinachohitajika ni wakenya kueza kuelimishwa pia kuhusu yaliyomo kwenye ripoti hiyo ,mswada huo wa BBI unapowasilishwa kwenye mabunge ya kaunti.
Sifuna amesema haya hii Leo kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio humu nchini .
Ameongeza kwamba kama chama cha ODM wiki ijayo watafanya kikao na wawakilishi wadi wa chama hicho , kuona kwamba wanapata nafasi kufahamu mengi pia kuhusu BBI.
Kuhusu kauli ya rais uhuru Kenyatta hivi maajuzi kwamba Kenya inapoteza shilingi bilioni mbili kila siku,sifuna amekariri kwamba ni jukumu la rais kuhakikisha kwamba anazuia swala la ubadhirifu wa pesa
Haya yanajiri huku mabunge ya kaunti sasa yakiwa na jukumu kujadili ripoti hiyo Chini ya miezi mitatu .
Story by Kennedy Babangida