Wakulima katika eneo la kimama kaunti ndogo ya Cheptais eneobunge la Mlima Elgon wamehimizwa kukumbatia mradi wa ufugaji wa kuku kama njia mojawepo  itakayowawezesha kujiondoa kwenye lindi la umasikini.

Akihutubu wakati wa kupeana malipo kwa wakulima afisa mkuu mtendaji wa chama cha ushirika cha kimama Ben Mulupi amedokeza kuwa wamepokea mtambo, wa kuangua zaidi ya mayai mia tano huku akiwasihi wakulima kujiandaa kwa mradi huo anaosema utawafaidi pakubwa.

Aidha mulupi ametoa wito kwa wakazi wa eneo hilo  kuzingatia masharti ya wizara ya afya katika juhudi za kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.

Ametumia fursa hiyo kuwahimiza wakulima wa kahawa kutunza mmea huo kwa njia inayofaa iwapo wanatarajia malipo bora. 

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE