Huenda wakulima wa miwa katika eneo la Magharibi wakapata afueni baada ya mwekezaji mpya almaarufu Devki, ambaye pia amewekeza katika sekta zingine kutarajiwa kuwekeza shilingi bilioni  5  ili  kukifufua kiwanda cha sukari cha Mumias kilichokuwa  kitega uchumi eneo hilo.

Akizungumza kwenye hafla ya mkutano wa wajumbe wa chama cha ANC katika kijiji cha Shibuli eneo bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega, mbunge wa Lugari Ayub Savula amesema kuwa wakulima wa miwa katika eneo hilo wameteseka kwa muda mrefu chini ya makampuni ya kibinafsi ya sukari kama vile West Sugar na kusema kuwa wakulima hao watapata nafuu baada ya mwekezaji mpya kujitokeza kukifufua kiwanda cha sukari cha Mumias ambacho wengi walikuwa wanakitegemea kimaisha.

Ni kauli iliyotiliwa mkazo na mbunge wa Lurambi askofu Titus Khamala ambaye amesisitiza changamoto wanazopitia wakulima wa miwa chini ya  kampuni za kibinafsi kama vile ugumu wa kupata leseni, kuongezeka kwa ufisadi na hata miwa kuharibikia mashambani jambo analodai linaendeleza umaskini katika eneo hilo.

Khamala aidha amechukuwa fursa hiyo kumpigia debe kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi na kusema  kuwa ni yeye tu ana maarifa ya kufufua sekta ya sukari na uchumi wa eneo la Magharibi na Kenya kwa jumla.

By Lindah Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE