Wito umetolewa  kwa wakulima kutoka kaunti  ya  Bungoma ambao huchukua mikopo katika shirika la kutoa  mikopo kwa wakulima  halmaarufu (  Agricultural Finance Corporation)  kulipa mikopo yao  kwa wakati ufao.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa  ujenzi wa afisi ya shirika hilo mjini Bungoma,mkurugenzi wa shirika hilo,George Kubai,amesema kuwa kuna haja ya wakulima  kuhakikisha kuwa mikopo wanayokopa wanalipa kwa wakati ufao bila kufuatiliwa huku akisema kuwa serikali haina mpango wowote wa kufutilia mbali madeni waliyonayo  .

Kwa upande wake waziri wa kilimo kaunti ya  Bungoma,Mathews Makanda,akiwataka wakulima kuekeza zaidi raslimali wanazopata kutoka kwa shirikahilo katika kilimo biashara ,akihoji hiyo ndiyo njia muhimu  itakayowawezesha kulipa mikopo yao bila tatizo  lolote.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE