Katika juhudi za kuimarisha utoshelezi wa chakula katika kaunti ya Kakamega, takriban wakulima elfu 24 wenye changamoto za kimapato wameanza kupokezwa pembejeo bila malipo kwa hisani ya serikali ya kaunti hiyo  huku fedha zaidi zikitengwa kuimarisha vyama vya mashirika kwenye kaunti hiyo.

Ni shughuli inayolenga akina mama tu wachochole wa kaunti ya Kakamega inaloendeshwa na Mawaziri wa serikali ya kaunti ya Kakamega, wakilishi wadi na maafisa wengine kuhakikisha kuwa walengwa wanafikiwa kabla ya msimu wa upanzi kukamilika.

Gavana wa kaunti hii Wycliffe Ambetsa Oparanya ameeleza kuwa serikali yake pia  imetenga kima cha shilingi milioni 25 kuviinua vyama vya ushirika katika kaunti ya Kakamega na nia ya kuimarisha uchumi na kuihakikishia kaunti hii utoshelezi wa chakula.

Tangu mwaka wa 2014, serikali ya kaunti ya Kakamega imekuwa ikitoa mbolea na mbegu kwa wakulima wake kwa bei ya chini, hili likiiimarisha zao la mahindi kwa takriban magunia milioni moja hadi kufikia sasa.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE