Wanaharakati chini ya vuguvugu la Bungoma Liberation wameilaumu serikali ya Kaunti ya Bungoma kwa kuwatoza ada za juu wahudumu wa Bodaboda licha ya hali ngumu ya uchumi.
Msemaji wa vuguvugu hilo Isaiah Sakonyi amemkashifu Gavana wa Bungoma Wycliffe Wangamati kwa kukiuka ahadi yake ya kuwaondolea mzigo wa ushuru wahudumu wa Bodaboda na wafanyabiashara wadogo wadogo.
By Hilary Karungani