Wahudumu wa bodaboda kutoka Embakasi, katika wadi ya Chesikaki eneobunge la Mlima Elgon wamejitenga na kisa ambapo vijana walijaribu kuvuruga mkutano ulioandaliwa na spika wa bunge la seneti Ken Lusaka wa kuchangisha fedha za kuvisaidia vikundi mbalimbali mjini Cheptais mwezi uliopita.

Wakiongozwa na ndiwa saima wanasema madai hayo ni ya kuharibia jina sekta ya bodaboda kutoka wadi ya Chesikaki ambapo wamejitenga kuhusika kurusha mawe kwenye  kanisa moja mjini Cheptais ambapo spika Lusaka alikuwa  mgeni wa heshima kwenye hafla hiyo.

Aidha wameilaumu serikali ya kaunti ya Bungoma kwa kile wanachodai kuwatelekeza hata baada yao kutimiza masharti ya kulipia stika za pikipiki.

Wanasema baadhi yao wanapitia hali ngumu kuendeleza masomo yao kando na kupokea huduma duni kutoka kwa ofisi za serikali na kutaka swala hilo kuangaziwa upesi.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE