Wahudumu wa bodaboda wa steji ya Melon katika wadi ya Chesikaki eneobunge la Mlima Elgon wameshiriki uchaguzi wa viongozi wao huku wakiahidi kutowahusisha vijana walio chini ya umri wa miaka kumina minane kwenye maswala ya biashara ya bodaboda.

Kulingana na Luka Wafula Wamalwa  ambaye amechaguliwa kwenye wadhifa wa mwenyekiti wa steji ya Melon ameahidi kuwatekelezea miradi mbalimbali ya maendeleo huku akidokeza kuwa hatowaruhusu vijana walio chini ya umri wa miaka kumina minane kujihusisha na biashara ya bodaboda.

Naye naibu mwenyekiti wao Lameck Wasing’ong’o akidokeza kuwa kamwe hawatakubali kutumiwa na wanasiasa kujinufaisha kando na kuwaahidi wanabodaboda uongozi ulio bora.

Aliyekuwa mwenyekiti wao Charles Nambuila akiwashauri viongozi ambao wamechukua hatamu ya uongozi  kuhakikisha wanatoa mwelekeo ulio bora na kutii sheria za trafiki.

By richard milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE