Wazazi katika kaunti ya Kakamega wameshughulika kuwapeleka watoto wao katika shule za upili huku wakilalama hali ngumu ya kiuchumi na kuwasuta baadhi ya walimu wakuu kushinikiza kuwa karo ilipwe yote

hata hivyo baadhi ya wanafunzi walipata afueni kwa kupata ufadhili wa mashirika na wahisani akiwemo michael maende wa shule ya msingi ya eshiakhulo eneo la Mumias Mashariki

Maende alipata alama 380 na kufanikiwa kupata ufadhili wa kujiunga na shule ya upili ya Booker kama anavyoeleza mwalimu mkuu wa Eshiakhulo Joshua Obuko

mwanasiasa wa Mumias Mashariki David Wamatsi ambaye alitoa ufadhili wa mahitaji kwa mwanafunzi huyo ameutaka usimamizi wa basari kuwapa umbele wanafunzi wanaojiunga na shule za upili ikizingatiwa hali ngumu ya maisha

Nayo familia ya mwanafunzi huyo kupitia kwa mamake Galdys Musungu wameelezea shukrani zao kwa ufadhili huo
By Lindah Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE