Baadhi ya wazazi katika shule ya upili ya Wasichana ya Cardinal Otunga kwenye Kaunti ya Bungoma wameushtumu uongozi wa shule hiyo kwa kuwatimua wanafunzi watano wa kidato cha tatu kwa madai ya kutumia dawa za kulevya.

Baadhi yao waliozungumza na Kituo hiki kwa njia ya simu, wameikosoa Bodi ya shule hiyo kwa kuwalazimisha wanafunzi kukubali makosa ambayo hawakuhusika na kuwatimua hata bila kuwapa nafasi kujieleza jinsi anavyoeleza mzazi huyu.

“Wanafunzi wanawekewa makosa tu na wanalazimishwa kuandika a false statement. Wanasema naibu wa mwalimu mkuu aliwalazimisha wanafunzi hao kuandika maelezo hayo na kuwatuma nyumbani na sasa sisi kama wazazi tumekuja kudhibitisha na tujakubaliwa kuingia”

Usemi wake umerejelewa na mzazi mwingine akisema ripoti ya daktari inaashiria kuwa mwanawe hajawahi tumia dawa za kulevya kinyume na makosa yanayomkabili.

“Tuko na maelezo ya daktari yanayoonyesha kuwa watoto wetu hawajatumia mihadarati sasa watoto hawa tutawapeleka wapi na hata hatujakubaliwa kuingia shuleni kama wazazi.”

Aidha wazazi hao wamedai kushurutishwa kulipa karo yote iliyosalia kabla ya kuruhusiwa kuondoka shuleni na wanao.

“Mwalimu mkuu ametuelezea tulipe karo na tumelipa yote lakini sasa hii pesa ya juu kando na karo turudishiwe ndo ata twende tutafutie watoto wetu shule nyingine.”

Kwa Jumla ni wanafunzi watano waliotimuliwa shuleni humo kwa madai ya kutumia dawa za kulevya na njama ya kupanga mgomo.

Story by Richard Milimu

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE