Wito umetolewa kwa vitengo mbalimbali humu nchini kushirikiana kikamilifu na wanahabari ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao inavyostahili hatua itakayowapa wananchi fursa ya kupokea taarifa zisizoegemea upande wowote.
Akihutubu baada ya kuongoza warsha kwa baadhi ya wanahabari kutoka kaunti ya Bungoma kwenye mkahawa mmoja mjini Bungoma Mashirikishi Kwa Baraza la wanahabari nchini MCK eneo la Magharibi Evans Teddy, amesema licha ya wanahabari kuwa nguzo muhimu kwenye jamii bado vitengo mbalimbali vinahujumu utendakazi wao na kuvitaka kuheshimu uhuru wao.
Wakati uo huo Teddy amedokeza kuwa lengo kuu la warsha hiyo ni kutoa mwelekeo kwa wanahabari namna ya kutekeleza majukumu yao pasi na kuhujumiwa na mtu yeyote.
Baadhi ya wanahabari wakiongozwa na Moses Masinde almaarufu Buffalo wakipongeza hatua ya baraza hilo kuandaa warsha hiyo na kuhakikisha wanazingatia matakwa ya wanahabari kikamilifu.
By Hillary Karungani