Mwanamke mmoja katika kijiji cha Magale, Lokesheni ndogo ya Bulovi lokesheni ya Kambiri iliyo katika wadi ya Isukha Kaskazini eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega amejifungua pacha watatu.

Velma Lukania mwenye umri wa miaka 19, ambaye ni mzaliwa wa kijiji jirani cha Sambakhalu mwanaye Magaret Anyango na marehemu Musa Muranda, anaitisha msaada kutoka kwa yeyote ili kutunza wanawe.

“Mimi nmejaliwa watoto watatu na namshukuru Mungu kwa zawadi ya watoto hawa. Hawa ni watoto wangu wa kwanza, sijawai zaa ata, sina usaidizi wowote wa kulinda hawa watoto. Ume wangu hana ata kazi na tunafanya kazi ya kulima tu sasa nmeamua kurudi kwetu nione kama mama yangu anaweza kunisaidia.”

Hata hivyo jamii aliyozaliwa ndani akiwemo dadake Velma, Quinter Atieno pamoja na mama mzazi Magaret Anyango wanaonyesha furaha yao kwa  pacha hao

“Tumeshukuru Mungu kwa watoto hao watatu lakini hakuna mtu wa kusaidia kwa maana ni watoto wavulana hata maziwa hakuna lakini tunajaribu kusaidia pale ambapo tunaeza.”

Watawala wa maeneo hayo patrick lumumba wa kijiji cha Magale, Evans Lisanza wa Imakuchi na Rita Juma wa nyumba kumi, wanaunga mkono kwa serikali kutoa usaidizi kwa jamii hiyo kwani kipato chao ni cha chini.

Story by Wycliffe Sajida

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE