Mbunge wa Sirisia John Koyi Waluke amewataka wakaazi wa eneo hilo kumuunga mkono kwa kufanya kazi kwa karibu naye kama njia pekee itakayomwezesha  kufanikisha ajenda ya maendeleo.

Akihutubu kwenye hafla ya mazishi eneo la Nabini wadi ya Lwandanyi eneobunge la Sirisia Waluke amehoji kuwa ushirikiano bora utamwezesha kutimiza ahadi mbalimbali kwa mwananchi huku akisisitiza umuhimu wa masomo kwa wanafunzi kando na kuahidi kuunganisha umeme  kwenye kijiji hicho.

Aidha Waluke ametumia fursa hiyo kuwasihi wakaazi wa eneo la Magharibi kwa jumla kujisajili kwenye chama cha U.D.A ambacho anasema kinazidi kuwa na umaarufu humu nchini.

Amewashauri wakaazi wa wadi ya Lwandanyi kufanya uamuzi wa Busara kwa kumchagua mwakilishi wadi atakayetekeleza miradi mbalimabli ya maendeleo kwenye uchaguzi mkuu ujao.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE