Walimu pamoja na washikadau wote katika sekta ya elimu wameshauriwa kuwa karibu na wanafunzi na kuwapa nafasi ya kujieleza ili kuepusha visa vya utovu wa nidhamu vinavyoendelea kushuhudiwa nchini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa mamlaka ya kudhibiti ubora wa elimu nchini (Kenya National Qualifications Authority) Dakt Juma Mukhwana, visa vingi vya utovu wa nidhamu vinavyoshuhudiwa katika baadhi ya shule vinaweza kuepukika kupitia ushauriano kati ya walimu, wanafunzi pamoja na wazazi.

“Wale tunaendesha shule tuwe na intelligence system ya kutosha na tukue proactive na nahimiza waalimu kukaa karibu na wanafunzi na kuzingatia somo la guiding and councelling kwa maana wanafunzu wanatoka pande na familia tofauti  na kwa hilo tutaweza kutatua shida mingi za utovu wa nidhamu kwa wanafunzi.” alieleza Mukhwana

Wakati uo huo, Mukhwana amependekeza wizara ya elimu kuajiri wanasaikolojia shuleni kama njia mojawapo ya kutatua matatizo ya msongo wa mawazao ambayo kwa nafasi kubwa yanasababisha visa vya utovu wa nidhamu shuleni ikiwemo migomo.

“Kwa sai tunatumia walimu kufanya guiding and cancelling na kulingana na vile wanafunzi wamekaa nyumbani kwa ajili ya korona walimu hawawezi kuendeleza guiding and counselling kwa sababu hawajapata maarifa ya kutosha kuendeleza usaidizi huo basi naomba serikali kuwajiri wanasaikolojia katika shule mbalimbali ili kusaidia wanafunzi ambao wako na msongo wa mawazo.”  alieleza

Mukhwana ameyasema  hayo katika hafla moja na washikadau katika sekta ya elimu  katika  eneo  ya  Kibabii.

Story By Hillary Karungani

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE