Shinikizo zinazidi kutolewa kwa rais Uhuru Kenyatta kuwahusisha viongozi wote wa kisiasa  kotoka eneo la Magharibi katika kupanga ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika eneo hilo mapema mwezi ujao.

Kulingana na mwanaharakati wa kisiasa katika wadi ya Mayoni eneo bunge la Matungu, Anerico Maero Junior, ingelikua vyema iwapo Rais Kenyatta angeandaa kikao na viongozi wote wa magharibi ili kubaini inayofaa anasema hatua ya rais kuwahusisha magavana pekee katika kupanga ziara yake inalenga kuwadunisha vigogo wa siasa kutoka eneo la magharibi akiwemo kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi.

Hata hivyo Anerico ambaye anamezea mate kiti cha mwakilishi wadi ya Mayoni katika uchaguzi mkuu ujao, amemtaka rais Kenyatta kulipa swala la ufufuzi wa kiwanda cha sukari cha Mumias kipao mbele atakapo zuru kaunti ya Kakamega. By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE