Huku kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka wa elfu mbili na ishirini na mbili kikisongea. Wanasiasa wengi wamejitosa kwenye kinyang’anyiro cha kiti cha Uwakilishi Wadi Katika Wadi ya Busali wote wakiwa na azima ya kuwaongoza wananchi wa Wadi hiyo.

Miongoni mwa wanasia hao ni akiwemo Bi. Florence Kegode ambaye mapema hii leo, ametawazwa rasmi kuwa mgombea wa kiti hicho Katika jamii ya Abagusui eneo hilo akisema yupo tayari kuwahudumia akipewa nafasi.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya Mwakilishi wadi hiyo Bi. Gladys Analo kuwarai wanawake wengi kujitosa kwenye ulingo wa siasa.

Wakati uo huo, wagombea wengine wakiongozwa naye aliyekuwa naibu chifu wa kata ya Bugina Aggrey Kidimu, wameonekana kuunga mkono Bi. Florence wakisema ni wakati wa jamii zingine eneo hilo kuongeza wadi ya Busali.

By Joseph Alovi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE