Mbunge wa Mlima Elgon Fred Chesebe Kapondi amewataka viongozi wa kisiasa waliochaguliwa kuwafanyia wananchi kazi kwa kuwatekelezea miradi mbalimbali ya maendeleo kama walivyowaahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.
Akihutubu kwenye hafla ya mazishi eneo la Toroso eneobunge la Mlima Elgon Kapondi amewahimiza wanasiasa kusitisha siasa za mapema na badala yake kuwahudumia wananchi kando na kuwashauri kuendesha siasa za amani.
Wakati uo huo kapondi amedokeza kuwa hivi karibuni kwa ushirikiano kati yake na dakta Sioyi watainua hadhi ya shule ya msingi ya Toroso ikiwemo kuanzisha bweni kwa wanafunzi wa kike ili kuinua viwango vya elimu miongoni mwa wanafunzi.
Amewataka wanasiasa kukoma kuendesha siasa kwenye hafla za mazishi.
By Richard Milimu