Muungano wa waanzilishi wa chuo Kikuu cha Sayansi na Technolojia almaarufu kama WECOFA wamegadhabishwa na hatua ya mahakama kuivunjilia mbali kamati kuu ya chuo hicho (Mmust Council) mwezi mmoja tu kabla ya sherehe ya kufuzu kwa wanafunzi waliohitimisha masomo yao mwaka huu

Mwenyekiti wa muungano huo Tom Shivachi akizungumza mjini Kakamega amemtaka gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Opranya, Mbunge Titus Khamala na viongozi kutoka kaunti hii kuingilia kati kuhakikisha kuwa uamuzi huo wa mahakama unaotishia kusambaratisha utendakazi wa chuo hicho unabadilishwa.

Amesema kuwa kusimamisha afisi kuu ya utendakazi katika chuo kutasitisha shughuli zote katika chuo ikiwemo sherehe za kufuzu na hili linatishia kukiua chuo hicho ambacho ni kitega uchumi kikuu kaunti hii ya Kakamega

Muungano huu umelaumu vyama vya kutetea maslahi ya wafanyikazi katika chuo hicho kwa kuchangia masaibu yanayokikumba chuo hicho ukidai wana njama fiche

Wametishia kushiriki maandamano ya amani kushinikiza kubatilishwa kwa uamuzi huo wa mahaakama

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE