Huku siku chache zikisalia watainiwa wa darasa la nane na kidato cha nne kukalia mtihani wa kitaifa mkurugenzi wa elimu kaunti ndogo ya Malava Isaac Kiprais amewahakikishia watahiniwa usalama wakati watakapokuwa wakiendelea na mtihani huo
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo la kanisa la marafiki mjini Malava Kiprais amewarai watainiwa hao kuwasili shuleni lisali moja kabla mtihani haujang’oa nanga.
Aidha mkurugenzi huyo amehoji kuwa wameweka mikakati kabambe ya kuzuia udanganyifu miongoni mwa wanafunzi