Afisa wa zamani wa maswala ya jinsia na watoto kaunti ya Kakamega Peninah Mukabane amehusisha visa vya baadhi ya wanafunzi kuukalia mtiani wao wakiwa hospitalini na mchecheto au exam fever
Kwenye kikao na wanahabari nyumbani kwake mtaa wa Emusala hapo jana Mukabane aidha amehusisha hali hiyo na baadhi ya ghasia za hivi punde ambazo zimeshuhidiwa kwenye baadhi ya shule humu nchini
Watoto walikaa nyumbai kwa mda mrefu hawakuwa na waalimu kwa karibu. Wako Na panic Na exam fever Na sasa wale ambao wako hospitali wamejifungua, naomba waalimu kuwaelewa na kuwaelekeza viluvyo
Haya yanajiri huku watahiniwa zaidi ya milioni moja wa shule za msingi wakitamatisha mtiani wao hapo Jana kupisha wenzao wa sekondari kuanza wao leo hii
Kwingineko watahiniwa wapatao 115 wa shule ya msingi ya Eshiakhulo wilayani Mumias Mashariki wamewashukuru wenzao wa zamani almaarufu alumni kwa msaada wa chakula pamoja na vifaa vingine vilivyowawezesha kuukamilisha mtiani wao
By James Nadwa